Giyorgis wa Segla

Giyorgis wa Segla alivyochorwa na Baselyos katika karne ya 17.
Tenzi za Giyorgis Kinanda cha Maria.

Giyorgis wa Segla (au wa Gesecha; 1365 hivi - 1 Julai 1425 hivi) ni kati ya Wakristo maarufu wa Ethiopia.

Alikuwa mmonaki, mtunzi wa tenzi na mwandishi wa vitabu kwa Kigeez aliyeathiri sana Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia, hasa upande wa liturujia na kalenda yake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Julai.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search